
Kikosi cha timu ya soka ya Yanga
Kocha mkuu wa mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka Tanzania bara Dar es salaam Young Africans mholanzi Hans Van der Pluijm amesema kila mchezo ulipo mbele yake katika ratiba ya ligi hiyo ni kama fainali kwa timu yake
Pluijm amesema hayo mara baada ya jana timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya timu ngumu ya Kagera Sugar toka mjin Bukoba katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam na kuiwezesha Yanga kuendelea kuifukuza Azam FC katika mbio za kuwania ubingwa msimu huu.
Pluijm amesema michezo miwili iliyobaki dhidi ya JKT Oljoro inayong’ang’ana kukwepa mkasi wa kushuka daraja na ule dhidi ya mahasimu wao Simba ni michezo muhimu kushinda na hivyo kwake ni kama fainali.
