Daniele de Rossi katika jezi ya taifa lake la Italia
De Rossi anayekipiga na AS Roma ya Italia alilazimika kuondoka uwanjani dakika ya 54 ya mchezo baada ya kuumia nyonga wakati timu yake ya taifa ikiwavua ubingwa Hispania kwa kuipa kipigo cha mabao mawili kwa sifuri.
Nafasi ya nyota huyo huenda ikachukuliwa na kiungo wa Juventus Giovanni Struaro ambaye inasemekana yupo tayari kwa ajili ya kuziba pengo hilo.
Kikosi cha Italia chini ya kocha Antonio Conte kimekuwa na matokeo mazuri katika hatua ya makundi ikifanikiwa kuzifunga Ubelgiji na Sweden .


