
Mwenyekiti wa IRFA Cyprian Myava amesema, timu zote mbili ya Lipuli FC na Kurugenzi zipo katika nafasi nzuri lakini anaona kuna tatizo katika uongozi ambapo wanatarajia kukaa kikao ndani ya wiki hii ili kuweza kutafutia ufumbuzi.
Myava amesema, hivi sasa wanazihamasisha timu ili kuweza kufanya vizuri ili ligi hiyo ikifika mzunguko wa pili timu hizo ziwe na uhakika wa kucheza Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara.
Myava amesema, Mashabiki na viongozi wa soka wanatakiwa kushikamana ili kuweza kukuza na kuendeleza soka katika mkoa huo.