Tuesday , 9th Dec , 2014

Bondia Iddy Bonge na Mussa Mbabe wanatarajia kupanda ulingoni katika pambano la Raundi 12 la kilo 70 pambano linalotarajiwa kufanyika Desemba 25 katika ukumbi wa Friends Corner jijini Dar es salaam.

Bondia Iddy Bonge

Akizungumza na East Africa Radio, Mratibu wa Pambano hilo, Mashaka Halfani amesema pambano hilo litakuwa ni la kumaliza ubishi kutokana na kila Bondia kutamani kukutana na mwenzake ili kujua ni nani zaidi katika ngumi.

Halfan amesema kabla ya kuanza kwa pambano hilo, kutakuwa na mapambano mengine 14 ya utangulizi kutoka kwa mabondia chipukizi.