Wednesday , 22nd Jun , 2016

Ureno iliyocheza kwa shida na kwa kujituma ili isihadhirike na kuishia hatua ya makundi ya Euro 2016, imetinga 16 bora baada ya kumaliza ya tatu kwenye mchezo wa kundi F.

Uingereza itacheza na Iceland kwenye hatua ya 16 bora ya michuano ya Mataifa ya Ulaya 2016 kwenye mji wa Nice jumatatu ijayo.

Iceland imemaliza nafasi ya pili ya kundi F, nyuma ya Hungary, baada ya kuadhibu Austria, mabao 2-1, na kuiacha Ureno kwenye nafasi ya tatu baada ya kulazimishwa sare ya mabao 3-3 dhidi ya Vinara.

Cristiano Ronaldo alifunga mara mbili, Ureno ikipata matokeo hayo ya kushangaza katika mechi ya tatu ikiwa haijashinda hata mechi moja na kuingia hatua hiyo ya mtoano, ambapo sasa itakutana na Croatia mjini Lens jumamosi hii.