Tuesday , 21st Jun , 2016

Mshambuliaji wa Sweden, Zlatan Ibrahimovic ametangaza kuwa atastaafu soka la kimataifa baada ya Euro 2016.

Ibrahimovic anatarajia kucheza mechi ya mwisho kwenye kundi E Euro 2016 kesho, ambapo itakuwa ni mechi yake ya mwisho katika nchi yake.

Aidha mshambuliaji huyo alikuwa amechaguliwa kuiwakilisha nchi yake katika mashindano ya Rio Olimpiki mwezi Agosti.

Hata hivyo klabu Manchester United walianza kujihusisha na mshambuliaji huyu mwenye umri wa miaka 34 alipokuwa mchezaji huru baada ya kuondoka katika klabu ya Paris St-Germain msimu huu.

Chanzo BBC