Tuesday , 12th Jul , 2016

Mlinda mlango wa Yanga Deogratius Munishi 'Dida' amesema hawawezi kuidharau timu ya Medeama katika mchezo wao utakaopigwa Jumamosi ya Julai 16 mwaka huu.

Mlinda mlango wa Yanga, Deogratius Munishi 'Dida'

Dida amesema, Medeama ni timu kubwa na ngumu tofauti na watu wanavyoifikiria lakini kikubwa watahakikisha wanapambana iloi kuweza kuibuka na ushindi.

Dida amesema, anaamini mchezo huo utakuwa na ushindani lakini kutokana na maandalizi ya uhakika wanayoendelea nayo wanaamini nafasi ya kufanya vizuri bado ipo.

Yanga na Medeama zitashuka dimbani kupambana katika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho litakalopigwa Uwanja wa Taifa jijini dar es salaam.