Thursday , 31st Dec , 2015

Kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara kinatarajia kuondoka hapo kesho kuelekea visiwani Zanzibar kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya Kombe la Mapinduzi linalotarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari Tatu mwakani.

Kocha msaidizi wa Klabu hiyo Juma Mwambusi amesema, michuano hiyo itakifanya kikosi hicho kiwe na uzoefu zaidi kwani wanatarajia kutumia kikosi kipana katika michuano hiyo.

Mwambusi amesema, walikuwa wasishiriki mashindano hayo lakini iliwalazimu kutokana na baadhi ya timu shiriki za michuano hiyo ambazo zinatoka nje ya nchi ambazo kwa upande wao itakuwa kama mechi za kirafiki.

Mwambusi amesema, kikosi kinamajeruhi ambao ni Amis Tambwe, Mbuyu Twite na Simon Msuva ambao mpaka sasa wanaendelea na mazoezi madogomadogo ili