katika kipindi cha miezi mitatu.
Hayo yamebainishwa na taarifa iliyotolewa na uongozi wa EATV LTD kwa kusema lengo la kuu la michuano hii ni kutaka kurejesha heshima ya mpira wa kikapu uliyopotea kwa kipindi kirefu.
"Mashindano haya yamekuwa yakiendeshwa katika Mkoa wa Dar es Salaam ambapo ndiyo wenyeji kwa mwaka huu 2017 na yamekuwa yakifanyika katika viwanja mbalimbali ndani ya Jiji, kwa lengo la kuufikisha mchezo huu mtaani ili kuibua na kupata vipaji vipya".
Kwa upande mwingine, michuano hiyo ya Sprite BBall Kings kabla ya kufikia hatua hii ya sasa iliweza kupitia katika sehemu takribani 5 ambazo ni Usajili, Mchujo kupata timu 18 bora, robo fainali, nusu fainali ambapo timu hizo ndiyo ziliweza kushinda na sasa zinakwenda katika kushuka dimbani kuminyana katika fainali.