Tuesday , 23rd Oct , 2018

Kituo Namba 1 kwa vijana EATV  kwa ushirikiano KWESE FREE SPORTS  tunayo furaha kubwa kuwatangazia watazamaji wetu kuanzia Jumapili ya  wiki hii tarehe 28 tutaanza kuonesha ‘LIVE’ mechi za ligi ya mpira wa kikapu kutokea Marekani NBA.

Nyota wa NBA, Lebron James (kushoto) na Stephen Curry (kulia)

Kila wiki tunatarajia kuonesha mechi mbili, na mechi ya kwanza ambayo tutaanza nayo Jumapili hii, itaanza saa 5 usiku kati ya Golden State Warriors na Brooklyn nets .

Endelea kutazama EATV, kusikiliza East Africa radio na kufuatilia mitandao yetu ya kijamii ili kupata taarifa zaidi.