Monday , 7th Dec , 2015

Chama cha mchezo wa wavu jijini Dar es salaam kimefuta mashindano maalum ya Uhuru ili kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ya kufanya usafi siku hiyo kuepusha mlipuko wa kipindupindu

Moja ya mechi ya mchezo wa wavu iliyofanyika jijini Dar ea salaam

Akizungumza na East Africa Radio mwenyekiti wa DAREVA Sirahu Mwasa amesema ni vyema wao kama wanamichezo wakashiriki kwenye zoezi hilo la usafi ili kuweka mazingira safi na kuepusha hatari ya mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.

Mwasha ameongeza kuwa baada ya kufuta mashindano hayo wao kama chama wanajipanga kwa ratiba ya mwaka ujao ambao wamepania kuboresha zaidi ligi ya mchezo huo iweze kufana zaidi ya ilivyokuwa mwaka huu.

Ameongeza kuwa wamejifunza mengi mwaka huu juu ya uendeshaji wa ligi hivyo lengo lao ni kuhakikisha mapungufu yaliyojitokeza yanarekebishwa na kufanya mashindano kuwa ya ubora wa kipekee mwakani.