Thursday , 21st May , 2015

Chama cha mpira wa kikapu mkoani Dodoma DARBA kimesema kinaendelea kutoa ushirikiano kwa vyuo vikuu vinavyoshiriki mchezo huo ikiwa ni pamoja na kuendeleza ligi ya vyuo inayoendelea mkoani humo.

Akizungumza na East Africa Radio, katibu mkuu wa DARBA, Benson George amesema, ili kuweza kudumisha ushirikiano huo, wanatarajia kuandaa mashindano maalum yatakayoshirikisha vyuo mbalimbali mkoani humo pamoja na vilabu ili kuweza kupata vipaji zaidi katika mchezo huo.

George amesema, mchezo wa kikapu mara nyingi umekuwa ukichezwa katika vyo vikuu kutokana na fursa iliyopo mkoani hapo ya kuwa na vyuo vingi ambapo wanaamini kwa fursa hiyo watapata vipaji vingi vya mchezo huo kutoka mkoani humo ambavyo vitaweza kuunda timu ya taifa.