Thursday , 18th Jun , 2015

Kocha msaidizi wa Klabu ya Yanga SC Boniface Mkwasa amesema, wanaendelea na mazoezi ambapo mpaka sasa Andrey Coutinho na Kpah Sherman wameshajiunga na kikosi kwa ajili ya kuendelea na mazoezi huku wakimpandisha mchezaji mmoja kutoka kikosi B.

Akizungumza na East Africa Radio, Mkwasa amesema, kwa upande wa mchezaji Raia wa Sierra Leone Lansana Kamara ambaye yupo katika majaribio hawawezi kumpima kwa mazoezi kama anafaa lakini wanaamini watapata majibu katika mechi za majaribio.

Mkwasa amesema, wamejaribu kujenga ukakamavu na kukazania masuala ya kiufundi pamoja na kutengeneza mambo ya msingi katika mpira kwani lengo lao ni kufanya vizuri mwanzo mpaka mwisho katika mashindano mbalimbali.