Friday , 15th Aug , 2014

UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga umeizidi kete klabu ya Simba SC baada ya kumsajili kiungo kati wa timu ya Gormahia ya nchini Kenya,Rama Saluma Mohamed aliyekuwa akiwaniwa na klabu hiyo.

UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga umeizidi kete klabu ya Simba SC baada ya kumsajili kiungo kati wa timu ya Gormahia ya nchini Kenya,Rama Saluma Mohamed aliyekuwa akiwaniwa na klabu hiyo.

Rama ametua kwenye klabu ya Coastal Union juzi akitokea nchini Kenya na kusaini mkataba wa kuitumikia timu hiyo kwa kipindi cha mwaka
mmoja.

Rama aliyewahi kuicheza timu hiyo kwa mafanikio makubwa na kufanikiwa kupata namba kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Kenya Harembee Stars alitua jijini Tanga juzi usiku akiwa na kulakiwa na viongozi wa klabu hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana,Katibu wa Coastal Union,Kassim El Siagi alisema kikosi cha cha timu hiyo msimu ujao kinatarajiwa kuwa tishio kutokana na kufanya usajili wa nguvu ambao unaonekana utaleta upinzani mkubwa sana.

“Ninachoweza kusema kikosi chetu msimu ujao kitakuwa tishio kwa sababu tunamatumaini makubwa ya kufanya vizuri kutokana na usajili imara ambao tumeufanya kwa kusajlili wachezaji nyota kama vile Obina,Shabani Kado Sued Tumba “Alisema El Siagi.

Alisema bado wanaendelea na mchakato wa kuhakikisha wanaimarisha kikosi hicho kwa ajili ya maandalizi ya kuelekea msimu mpya wa ligi
kuu Tanzania bara msimu ujao.

KIBUTA AANZA KUONYESHA CHECHE ZAKE COASTAL UNION.

BEKI wa kulia wa Coastal Union,Suleiman Kibuta ameonekana kuwa mwiba mkali katika mazoezi ya timu hiyo yaliyo chini ya Kocha mkuu wa timu
hiyo Yusuph Chippo kwa kutoa pasi nzuri za mara kwa mara na kufanikisha upatikanaji wa mabao.

Mazoezi hayo hufanyika kila siku kwenye viwanja wa Mkwakwani mkoani hapa yakihusisha mazoezi mbalimbali ikiwemo kukimbia,kufanya mazoezi
ya viungo na kucheza mechi ya pamoja.

Kibuta ambaye alisajiwa na Coastal Union msimu huu akitokea klabu ya Kagera Sugar ya Bukoba amehaidi kuipa mafanikio timu hiyo katika
harakati zake za kuwania ubingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara msimu ujao.

Alionekana kuwa gumzo mara kwa mara alipokuwa akimilika mipira aliyokuwa akipewa pasi na wachezaji wenzake kwa kucheza kwa umahiri
mkubwa hali iliyopelekea mashabiki wa soka waliohudhuria mazoezi hayo kulipuka kwa shangwe.

Alisema kuwa kusajiliwa kwake kwenye timu hiyo ni faraja kubwa saa hivyo atahakikisha anashirikiana na wachezaji wenzake lengo likiwa
kikosi hicho kinakuwa tishio kwenye mashindano ya ligi kuu soka Tanzania bara ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi mwezi septemba
mwaka huu.

“Unajua mimi muda mrefu nilikuwa na ndoto za kuja kukipiga kwenye timu hii ya Coastal Union hivyo baada ya kusajiliwa nimepata ridhaa ya
kuicheza nitapigana kufa na kupona niweza kutoa mchango wangu utakaokuwa na matokea makubwa “Alisema Kibuta.

Kibuta ni miongoni wa wachezaji wenye histori kubwa ya soka hapa nchini aliyepitia vilabu vya Simba,Moro United na Maji Maji ya Songea
alivyovichezea kwa mafanikio.