Akizungumza na East Africa Radio, Mwenyekiti wa CHANETA, Anna Kibira amesema wenyeviti wa mabaraza ya michezo wanatakiwa kuungana na kuandaa bajeti kuhakikisha timu zinashiriki katika mashindano hayo.
Kibira amesema, iwapo mashindano ya kanda yatasimamiwa kikamilifu, wanaamini wataweza kupunguza gharama kubwa zinazotokana na uandaaji wa mashindano ya ya Taifa.
Kibira amesema, baada ya kumaliza michuano ya Taifa iliyokuwa na changamoto mbalimbali zilizojitokeza, wanatarajia kukutana na kamati ya utendaji kwa ajili ya kufanya tathimini.
Kibira amesema michuano hiyo ilishirikisha timu zilizokuwa na vijana ambao walileta changamoto kwa timu mbalimbali zilizoshiriki katika michuano hiyo.