Makamu mwenyekiti wa CHANETA Zainab Mbilo amesema kuwa kitu kingine ambacho ni cha kupongezwa ni kwa kuongezeka kwa timu za wanaume katika michuano hiyo kwani awali kulikua na timu mbili pekee
Mbilo amesema kuwa msimu huu umekua wa neema kwao kama wenyeji kwani timu nane za wanaume zinashiriki michuano hiyo na zimeonyesha uwezo mkubwa na pia waamuzi nao amewapongeza kwa kuchezesha kwa kufuata sheria za mchezo huo kitu ambacho kimepelekea kutokuwepo kwa malalamiko makubwa juu ya maamuzi katika michezo iliyokwishachezwa.