Mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa kimichezo Cas imepokea rufaa 11 kutoka kwa wanariadha wa Urusi waliofungiwa kushiriki Olimpiki, wakiwa tayari wameshapiga kambi ya muda mjini Rio.
Rufaa zingine 7 kutoka kwa waendesha makasia na waogeleaji zimeahirishwa, huku chama cha cha wanyanyua vitu vizito nacho kikiwakilisha rufaa, baada ya shirikisho la wanyanyua vitu vizito kuifungia timu ya Urusi ambayo ilishawasili Rio, wiki iliyopita.
Cas itafanya maamuzi ya kuhusu hatama ya timu za Urusi za michezo ya kupiga makasia baharini na kunyayua vitu vizito, kuanzia leo na kesho.
Kamati ya kimataifa ya Olimiki IOC iliiruhusu Urusi kupeleka wanamichezo wake kwenye Olimpiki, lakini endapo wakiwa hawajawahi kufungiwa na kashfa ya utumiaji wa dawa zilizopigwa marufuku michezoni.





