
John Bocco
Taarifa kutoka kwa moja wa viongozi klabuni hapo zinasema kuwa baada ya nahodha huyo kuumia katika mchezo ule, alipelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu pamoja na kufanyiwa uchunguzi, na leo majibu wa daktari wa timu hiyo yanaonesha kuwa alichanika nyama za paja, hivyo atatakiwa kukaa nje ya dimba kwa muda wa wiki mbili.
Siyo Bocco peke yake ambaye alikumbwa na dhoruba katika mechi, bali pia kiungo wao mkata umeme raia wa Cameroon, Stephen Kingue Mpondo pia alipata majeraha na ripoti hiyo inapendekeza aungane na Bocco katika kujiweka sawa kwa muda wa wiki mbili kabla ya kurejea dimbani.
Hii ina maanisha kuwa wachezaji hao wawili watakosa mechi mechi mbili, dhidi ya Ndanda FC (Februari 4) na dhidi ya Ruvu Shooting.
Ikumbukwe kuwa Bocco ndiye aliyepeleka msiba Msimbazi kwa kufunga bao pekee lilipa Azam point 3 katika mchezo huo.