Tuesday , 22nd Nov , 2016

Baraza la Michezo nchini limevitaka vyama vya riadha vya mikoa kufanya uchaguzi kabla ya Novemba 27 mwaka huu ili kuweza kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa Chama Cha Riadha nchini RT

Wanariadha Tanzania

 

Afisa habari wa BMT Najaha Bakari amesema, vyama vya mikoa ndivyo vinavyotarajiwa kupiga kura katika uchaguzi wa RT ambao utafanyika Novemba 27 mwaka huu jijini Dar es salaam na wamekwishawaandikia barua ya kuwataka kufanya uchaguzi katika vyama vyao ili kuwawezesha kupiga kura katika uchaguzi Mkuu.

Najaha amesema, usaili kwa wagombea wote waliochukua fomu za ugombea wa nafasi mbalimbali ndani ya Chama hicho utafanyika Novemba 26 ambayo ni siku moja kabla ya uchaguzi na wapiga kura watapiga kura kwa kutumia utaratibu wa NDIYO au HAPANA kwa kila nafasi yenye mgombea mmoja.