Baaada ya kuenguliwa kwenye michuano ya Olimpiki ya mwaka huu itakayofanyika mjini Rio de Janairo nchini Brazil, Shirikisho la ngumi za ridhaa Tanzania, BFT limetangaza kuendelea na program zake za mashindano.
Makamu wa rais wa BFT, Lukelo Wililo amesema tayari wameshaanda program hiyo na wanaamini michuano yote waliyoidhamiria itafanyika kwa wakati ikiwepo ile ya ngazi ya taifa itakayofanyika hivi karibuni.
Wililo amesema michuano ya ngazi ya taifa wamepanga ifanyike jijini Dar es salaam ambapo wanaamini ni sehemu sahihi kwa timu zote za Mikoa kufika kwa wepesi.






