Thursday , 14th Aug , 2014

Basi la Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limekamatwa na madalali kwa amri ya mahakama kutokana na deni la sh milioni 140 ambalo inadaiwa hadi litakapolipwa.

Ofisi za zamani za Shirikisho la Soka Tanzania TFF

Basi la Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limekamatwa na madalali kwa amri ya mahakama kutokana na deni la sh milioni 140 ambalo TFF inadaiwa hadi litakapolipwa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka TFF, amri hiyo imetokana na deni hilo la kampuni ya Punchline ya Kenya iliyokuwa ikichapa tiketi za kuingilia uwanjani kuanzia mwaka 2007.

Kwa upande wao TFF inasema kuwa hadi sasa imekwishalipa sh. milioni 70 katika deni hilo na inaendelea na Jitihada ili kumaliza deni hilo

Pia TFF imesema kuwa inachunguza mwenendo mzima uliosababisha kuwepo deni hilo.