Friday , 25th Apr , 2014

Timu ya Tanzania Bara imeibuka bingwa katika mashindano ya mpira wa meza ya kombe la muungano yaliyoshirikisha timu kutoka Tanzania Bara, Zanzibar na wageni waalikwa Zambia.

Meza ya table tenis, mchezo unaokua kwa kasi Tanzania.

Akiongea mara baada ya kumalizika mashindano hayo, Mwenyekiti wa chama cha mpira wa meza Tanzania (TTTA), Felix Maganjira, amesema kufanikiwa kwa mashindano hayo ni mwanzo mzuri wa chama hicho kuelekea michuano ya Jumuiya ya Madola.

Kwa Upande wao, wachezaji wakongwe walioshinda katika mashindano hayo kwa wanaume na wanawake, Yahaya Mungira na Agnes Ngodoki, wanasema uzoefu wao ndio uliowawezesha kuibuka washindi katika michuano hiyo.