Nahodha mpya wa timu ya Taifa ya kriketi ya Afrika Kusini AB de Villiers amesema hana uhakika kama ataendelea kuwa kiongozi baada ya kumalizika mashindano ya Test dhidi ya Uingereza.
De Villiers, 31, amerithi mikoba ya Hashim Amla, ambaye alijiuzulu baada ya Test ya pili dhidi ya Uingereza huko Cape Town wiki iliyopita.
De Villiers amesema "Matazamio yangu ni kwenye kriketi ya kimataifa na ninataka nicheze kwa kipindi kirefu," alisema De Villiers.
Iliarifiwa mwezi Desemba mwaka uliopita kuwa De Villiers atatundika daluga kwenye kriketi baada ya mashindano ya Test, lakini nahodha huyo amekanusha uvumi huo.
De Villiers, ni nahodha wa Afrika Kusini wa timu ya One-Day tangu 2012 na amecheza Test 104 na One-Day Internatinal 195 tangu aitwe kwa mara ya kwanza mwaka 2004.
Afrika Kusini itaingiaTest ya tatu hapo kesho huko Johannesburg, huku Uingereza ikiongoza 1-0, katika mtiririko wa mechi 4.


