Aliyekuwa kipa wa Azam FC, Mwadini Ali
Afisa habari wa Azam FC Jaffery Iddy Maganga amesema, Klabu ya Simba ilituma barua kwa lengo la kuwahitaji wacheza hao na wameshakubaliana kwa ajili ya kuwatoa kwa msimu mmoja kuitumikia klabu hiyo.
Jaffery amesema, wachezaji hao watajiunga na klabu ya Simba iliyo mkoani Morogoro kwa ajili ya kambi ya maandalizi ya Ligi kuu ya soka Tanzania Bara.
Wiki iliyopita Simba ilileta wachezaji wawili kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kiungo Sanga Bahende na mshambuliaji Cedrick Masanga, wote kutoka FC Lupopo ya Lubumbashi.
Wakongo hao walifanya idadi ya wachezaji wa kigeni waliokuja kwa majaribio Simba kufika saba, baada ya mabeki Mzimbabwe, Method Mwanjali, Janvier Besala Bokungu, kiungo Mussa Ndusha wote kutoka DRC, washambuliaji Frederick Blagnon kutoka Ivory Coast na Ndjack Anong Guy Serges kutoka Cameroon.
Mbali na wachezaji hao wa kigeni, kuna wapya wengine ambao ni pamoja na watatu waliosajiliwa kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro, wote viungo Muzamil Yassin, Mohamed ‘Mo’ Ibrahim na Shizza Kichuya na Jamal Mnyate kutoka Mwadui FC.
Wengine ni Moses Chibandu, Said Mussa, Kelvin Falu, Vincent Costa wote wapya pamoja na wa zamani Nahodha Mussa Hassan Mgosi, Juuko Murshid, Vincent Angban, Awadh Juma, Said Ndemla, Peter Mwalyanzi, Peter Manyika, Dennis Richard, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hijja Ugando, Novatus Lufunga, Mwinyi Kazimoto, Danny Lyanga na Ibrahim Hajib.





