
Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa alipokuwa anazungumza na wanahabari katika makao makuu ya ofisi zao za Kaunda, Jangwani na kusema amempokea kijana wake huku akimwagia sifa kuwa ana 'discpline'.
“Mchakato unaoendelea sasa hivi unajulikana na sisi tunafanya mambo yetu kimya kimya na yakishakamilika ndiyo tunayaweka hadharani. Kwa hiyo leo tunamtambulisha mchezaji aliyekuwa kwenye rada zetu kwa siku nyingi na nadhani wote mnamfahamu, tunamtambulisha rasmi kwa wapenzi wa Yanga na wanamichezo wote kwa ujumla mchezaji Ibrahim Ajibu ambaye kuanzia hivi sasa amepata kandarasi ya kuchezea klabu yetu ya Yanga kwa kipindi cha miaka miwili", amesema Mkwasa.
Mpaka sasa Yanga wamefanikiwa kuwa winda wachezaji watatu kutoka nje ya timu yake ambao ni Abdallah Haji Shaibu "Ninja" kutokea timu ya Taifa ya Jang"ombe, Pius Buswita akitokea mbao Fc pamoja na mshambuliaji Ibrahim Ajib kutokea wekundu wa msimbazi Simba.