Wednesday , 8th Apr , 2015

Kocha wa Timu ya Taifa ya Vijana chini ya Miaka 15, Adolf Richard amesema hivi sasa anaangalia mapungufu yaliyopo katika kikosi hicho.

Akizungumza na East Africa Radio, Richard amesema anaangalia vijana hao wana ufundi gani ndipo aweze kuelewa ni wapi anaanza ili kuweza kuboresha kipaji kilichopo.

Richard amesema, mapungufu yaliyopo yanaweza kuondoka kwa muda kwani programu ni ya muda mrefu na anaamini njia kuu mbili za mpira zitatumika na kueleweka kwa kila kijana.

Richard amesema, katika kukuza na kuelewa vipaji vya vijana hao watakuwa na mechi za kirafiki na wataweza kuchuja vijana na kuweza kupata vijana wenye vipaji ambao watakuwa na uwezo wa kuwa katika kambi hiyo.