
Kocha msaidizi wa timu hiyo Edna Lema amesema, watakuwa na mazoezi ya siku 10 kwa ajili ya mazoezi na mechi dhidi ya Malawi wanaamini watajifunza na kupata uzoefu pamoja na kuangalia mapungufu yaliyo ndani ya timu hiyo ili kuweza kuyafanyia marekebisho.
Kocha Edna amesema, walitarajia kuwa na kikosi cha wachezaji 28 lakini wachezaji watatu wapo katika maandalizi ya mtihani wa taifa wa kidato cha nne na katika kikosi hicho kuna baadhi ya wachezaji ambao ni wapya na wapo kwa ajili ya kuongeza nguvu katika kikosi hicho.