Wednesday , 28th May , 2014

Rapa mwenye umri mdogo na kipaji kikubwa katika gemu ya muziki Tanzania, Young Killer, leo hii ameshiriki 'Kikaangoni Live', katika ukurasa wa facebook wa EATV akipangua maswali mengi ambayo wadau na mashabiki wake walikuwa na kiu ya kufahamu.

Msanii wa Hip Hop Tanzania Young Killer

Young Killer ambaye ndiye msanii bora chipukizi wa mwaka huu, katika muda wa saa mbili amejibu maswali ambayo pia mengine yamekuwa ni msaada kwa kuonyesha njia kwa wale wote wanaomfuatilia, katika harakati zake za kila siku za kimaisha.

Baadhi ya maswali yaliyokuwa ni changamoto kwake ni kuhusiana na mashabiki wake kutaka kujua kazi zake mpya kutokana na wengi kumkubali haswa kwa nyimbo yake ya 'Dear Gambe' aliyomshirikisha msanii Belle 9.

Hivi sasa macho yote yanaitazama wiki ijayo kwa hamu kubwa kufahamu atakuwepo staa gani kwa ajili ya kuchat nae LIVE, endelea kuifuatilia, like na share na marafiki ukurasa huu wa www.facebook.com/eatv.tv kwa burudani kama hii na nyingine kali.