Wednesday , 29th Jul , 2015

Staa wa muziki Young Killer, aliyejijengea kutokutabirika katika aina ya wasanii ambao huwa anawashirikisha katika ngoma zake, ameweka wazi kuwa, huwa anazingatia zaidi uwezo wa mtu na kile ambacho kitawezesha ngoma yake kudumu kwa muda mrefu.

staa wa miondoko ya bongofleva nchini Young Killer

Kwa kufuatilia kolabo ambazo Young Killer tayari amekwishawahi kufanya, staa huyo akionekana kuwa na umakini kuchagua mtu wa kufanya naye kazi, akitolea mfano wa miezi mingi aliyotumia kumsubiri msanii Maua kwa ajili ya projekt yake mpya kutoka na vigezo alivyovitaja.