Monday , 2nd Mar , 2015

Staa wa Muziki Young Dee, ametangaza kuwa katika mpango wa kuanza kuwachukulia hatua wasambazaji wa kazi za wasanii mtandaoni ambao huzichukua kazi zao kutoka katika mfumo wa kulipia na kuziweka wazi kwa kila mtu kuzipata bure.

msanii wa bongofleva nchini Young Dee

Young Dee amesema haya baada ya kuweka wazi kilio chake kwa wasambazaji hawa mtandaoni hivi karibuni, akitaka wafahamu kuwa utaratibu huo ni kosa kisheria na unawarudisha nyuma wasanii ambao wanajaribu kujitengenezea mapato kwa njia ya mtandao.