Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Mbogo Futakamba.
Akizungumza wakati wa kupokea dawa hizo Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Mbogo Futakamba, amesema kuwa serikali imejipanga kuhakikisha hadi kufikia mwaka 2020 asilimia 85 ya wakazi wanaoishi maeneo ya vijijini wawe wanapata huduma ya maji safi na salama.
Mhandisi Futakamba amesema licha ya kuhakikisha asilimia hizo kwa wakazi vijijini lakini wamejipanga pia kuhakikisha asilimia 90 ya wakazi waishio mijini wanapata huduma hiyo ya maji safi na salama.
Kwa upande wake Mwakilishi wa WHO, nchini Dkt. Richard Banda amesema kuwa shirika hilo limeamua kutoa dawa hizo ili kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu ambao ni tatizo lililolikabili nchi ya Tanzania kwa kipindi cha mwaka mmoja sasa.
Tafiti zinaonesha kuwa kuanzia mwezi Agosti mwaka 2015 hadi sasa zaidi ya watu 22 elfu wameugua ugonjwa huo na wengine 347 wamefariki dunia baada ya kuugua ugonjwa wa kipindupindu.
Miongoni mwa halmshauri zitakazopata dawa hizo ni pamoja na, Ngorongoro, Monduli, Chamwino, Meru,Kondoa, Kongwa, Bukombe, Kilolo, Karagwe, na Kasulu.