Friday , 2nd Nov , 2018

Baada ya kuwepo na stori kwamba wasanii kutoka kundi la Weusi wamechangia kwa kiasi kikubwa kupoteza tamaduni za Arusha kwenye muziki wao, msanii G Nako amekanusha taarifa hiyo na kusema mitindo ni jinsi wewe unavyo vaa.

Wasanii wa kundi la Weusi.

Akiongea kupitia eNEWZ  G Nako amesema kwamba  mitindo ni jinsi unavyojiweka wewe mwenyewe na hata wao huwa wanajitahidi kuvaa na kuonyesha mitindo ya ki Arusha kwa baadhi ya sehemu na sehemu nyingine inabidi wavae kutokana na mahali husika.

G Nako ameendelea kusema kwamba "tunajitahidi kwenda na wakati ili kuweza kuwapa mashabiki zetu ladha mbalimbali katika sanaa kama unavyojua sisi ni wasanii na tunapaswa kubadilika kutokana na mazingira yanayokuwepo".

Pia G Nako kwa sasa anatamba na wimbo wake mpya unaoitwa Tingisha ambao amemshirikisha msanii mgeni wa kike ambaye ndo anachipukia na kusema kwamba alikutana na msanii huyo studio na baada ya kuona anakipaji akaona ampe shavu kwenye nyimbo yake hiyo.