Thursday , 13th Nov , 2014

Kundi la muziki la Weusi limeahirisha onyesho lao kubwa la Funga Mwaka lililokuwa limepangwa kufanyika tarehe 14 huko jijini Mbeya, kupisha msiba wa mwana hip hop Geez Mabovu aliyefariki dunia siku ya jana.

wasanii wa kundi la muziki la Hip Hop nchini Weusi

Msemaji wa kundi la Weusi Nikki wa Pili amewataka mashabiki wa kundi hilo kufahamu kuwa, wao hufanya kazi ya kurap kwa kutafuta heshima na si pesa kwanza huku akitoa salamu za rambi rambi kwa kifo cha msanii huyu.

Tarehe mpya ya kufanyika kwa onyesho hili itatangazwa hapo baadaye baada ya kupoa kwa majonzi na pigo hili kubwa katika sanaa ya muziki Bongo.