Friday , 7th Nov , 2014

Burudani ya aina yake imepangwa kuwaangukia wakazi wa Moshi siku ya kesho ambapo kundi zima la Weusi litadondoka katika Club ya La Liga kwa ajili ya onesho kubwa la Funga Mwaka kwa mashabiki wao mkoani humo.

kundi la muziki Weusi la nchini Tanzania

Katika onesho hili, Weusi watasindikizwa jukwaani na wasanii Belle 9 pamoja na AY katika kuhakikisha kuwa ladha mbalimbali za muziki zinaongeza chachu katika onesho hilo la aina yake.

Kiingilio katika onesho hili kubwa, kitakuwa ni shilingi 10,000/= tu mlangoni.