Wednesday , 1st Oct , 2014

Leo hii, siku 03 tu zikiwa zimebaki kufikia fainali za mashindano ya Dance 100 2014, kundi linalofahamika kama Wazawa Crew limekutana na eNewz na kufunguka kwa undani juu ya mashindano haya kwa mwaka huu na makakati kuelekea ushindi siku ya fainali.

shindano la kucheza muziki la Dance100% 2014

Kundi hilo lenye umachachari wa kusakata dansi, katika mahojiano yake na eNewz likajinadi kwa mashabiki wao namna lilivyojipanga ili kuhakikisha kuwa wao ndio wanaibuka washindi wa shindano hilo.

Siku zinaendelea kwisha, na macho yote ni kuelekea fainali za mashindano haya jumamosi hii, swali lenye uzito wa kutosha likibaki kuwa ni kundi litakalochomoka na mpunga milioni 5 kati ya The WT, Wakali sisi, Best Boys, Wazawa Crew na The winners Crew.