Friday , 11th Nov , 2016

Kituo cha East Africa Television leo kimekamilisha zoezi la kutaja wasanii wote wanaoshiriki katika Tuzo za Muziki an Filamu za EATV Awards kwa kutaja 'nominees' wa vipengele vitatu vilivyokuwa vimebakia

Wawakilishi kutoka EATV, Baclays, BASATA, Vodacom na Innovate katika mkutano na wanahabari.

 

Kupitia mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Hoteli ya Slipway jijini Dar es salaam, EATV LTD ikishirikana na Vodacom Tanzania, CocaCola, Barcklays Bank, kampuni ya ukaguzi ya Innovate pamoja na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) imetaja vipengele hivyo vitatu, ambavyo ni mwanamuziki bora wa kiume, mwanamuziki bora wa kike na wimbo bora wa mwaka. 

Godfrey Mngereza - Katibu Mtendaji wa BASATA

 

Wasanii hao tukianzia na msanii bora wa kiume ni

G Nako - 'Original'

Shetta - 'Namjua'

Ben Pol - 'Moyo Mashine'

Mwana FA - 'Ahsanteni kwa kuja' 

Alikiba - 'Aje'

Kipengele kingine ni mwanamuziki bora wa kike, ambapo wasanii waliofanikiwa kuingia kwenye kinyang'anyiro ni 

Lilian Mbabazi - 'Yoola' (Uganda)

Ruby - 'Forever' 

Linah - 'Malkia wa nguvu'

Vanessa Mdee - 'Never ever'

Lady Jaydee - 'NdiNdiNdi'

Kipengele cha mwisho ambacho kilitangazwa washiriki wake leo kilikuwa ni wimbo bora wa mwaka, na nyimbo zilizofanikiwa kuingia ni kama ifuatavyo:

Don't Bother - Joh Makini 

NdiNdiNdi - Lady Jayde

Kamatia chini - Navy Kenzo 

Aje - Alikiba 

Moyo Mashine - Ben Pol 

Baada ya kutangazwa kwa vipengele hivyo tayari zoezi upigaji kura limefunguliwa kuanzia leo saa sita usiku kwa njia ya simu kupitia namba 15777 na njia ya mtandao kupitia tovuti ya eatv.tv/awards kwa utaratibu utakaotangazwa.

Zoezi hilo la upigaji kura litakamilika tarehe 8/12/2016.

Tags: