Monday , 18th Aug , 2014

Katika kuonesha moyo ya upendo na kujali, timu ya wasanii ambayo Jumamosi hii imewasha moto Mjini Dodoma katika tamasha la Kili Music, imepata nafasi ya kufika nyumbani kwa msanii Afande Sele Morogoro kumpa pole kwa kuondokewa na mzazi mwenzake.

wasanii wa muziki wakiwa na Afande Sele mkoani Morogoro

Miongoni mwa wasanii ambao wameshiriki katika zoezi hili lililofanyika jana ni pamoja na Ben Pol, Joh Makini, Izzo Business, Shilole Kiuno na Khadija Kopa kati ya wengine.

Ziara ya wasanii hawa kwa msanii huyu imekuwa ni faraja kubwa na pia ishara ya mahusiano mazuri pamoja na umoja kwa wasanii Tanzania.