Wakizungumza na EATV kwa nyakati tofauti, wasanii hao wamesema ni faraja kubwa kwao kufanikiwa kuingia kwenye tuzo hizo, kwani zimefanya watambulike zaidi na kuzitangaza kazi zao.
"Ruky Beby...."Nilipata shock nilipoambiwa nimechaguliwa kwenye EATV AWARDS, kwanza nililia kwa furaha huku mama yangu akinishangaa, binafsi sikuamini kwa sababu hii ndiyo kazi yangu ya kwanza na kwenye game sina muda, kwa kweli kwangu ni furaha sana".
Bright......" Kwangu ni furaha iliyopitiliza kwa sababu ni kitu ambacho sikutegemea, yani naweza sema ni furaha iliyopitiliza, hii inatusaidia na sisi tunatambulika".
Mayunga ....."Kwangu mimi hata sijui nielezeje, ndiyo tuzo za kwanza kushiriki na nikiwa msanii chipukizi bado, kilichobaki nawaachia tu mashabiki
Man Fongo...."Najisikia vizuri kwa mara ya kwanza kuingia kwenye tuzo, alafu ukizingatia aina ya muziki ninaofanya wa singeli, wengine hawaukubali kabisa, lakini namshukuru Mungu na mashabiki ndiyo watakao amua".
Ili kuwapigia kura wasanii hao, andika code zao halafu tuma kwenda namba 15777, au tembelea website yetu www.eatv.tv/awards