Tuesday , 13th Dec , 2016

Meneja wa muigizaji bora wa kike Afrika Mashariki Chuchu Hansy amesema wasanii wengi wa Tanzania wana mgando wa mawazo na ndiyo maana wanashindwa kufikiria mbinu mpya za kufanya kazi zao, na kubaki na movie zenye part (sehemu) kibao.

Meneja wa Chuchu Hansy

Meneja huyo alitoa kauli hiyo baada ya kupokea tuzo kwa niaba ya Chuchu Hansy kwenye Tuzo za EATV, alipoulizwa ni kwanini wasanii wa filamu nchini akiwemo Chuchu wasihamie kwe kutengeneza 'series'  (tamthilia) badala ya kukomaa na movie pekee, ndipo meneja huyo akatoa majibu huku akitaja tatizo kubwa walilonalo wasanii wa bongo movie.

Msikilize hapa ambapo alianza kuwa kuzungumzia mwenendo wa tasnia ya filamu tangu kuondoka kwa Steven Kanumba aliyefariki dunia mwaka 2012.

 

Tags: