Tuesday , 17th Feb , 2015

Marehemu Mzee Abby Sykes ameacha pengo kubwa lisilozibika katika tasnia ya burudani, huku akijibebea sifa kubwa ya kuwa kipenzi cha vijana hususani wale wanaojihusisha na sanaa ya muziki hapa Bongo.

Dully Sykes akiwa na Baba yake Marehemu Ebby Sykes Enzi za Uhai wake.

Kwa kulifahamu hilo, eNewz imeweza kuongea na baadhi yao na kuweza kusikia vile wanavyomzungumzia na kumfahamu marehemu Abby Sykes;

DITTO: "Namna ambavyo amekuwa akichukua uzoefu wake na kutupatia sisi sehemu tofauti tofauti ambazo tulikuwa tukikaa naye, ni mtu ambaye hakukaa mbali na sisi vijana, amekuwa ni mtu mzima ambaye alikuwa akitupa ushauri na vitu vingine, so kikubwa mimi nitamiss hivyo, na pia namna uimbaji wake na upigaji wake wa gitaa ulivyokuwa unatuvutia".

RICH MAVOKO: "Sikuwahi kukaa naye sana lakini nakutana naye sana kwahiyo nilikuwa namuona ni mtu wa peace na kila mtu, yani hilo kutoka moyoni kabisa,.. nilikuwa namchukulia mzee kijana, nilikuwa namtania 'Jembe'.

MALFRED: "Nakumbuka nilikuwa napiga Live na Mzee mwaka jana,.... ni mzee lakini kwa sisi vijana alikuwa ni kama rika letu kwa vile alivyokuwa anashare ideas za muziki na maisha ya kawaida ya kila siku'.

AY: "Ni mzee wetu na pia alikuwa ni rafiki yangu, alikuwa tukikutana tunaongea, tunabadilishana mawazo na vitu kama hivyo".

CHEGGE: "Namzungumzia kama baba wa kila msanii na vilevile naweza kumzungumzia kama kipenzi cha watu wengi kwasababu watu wote walikuwa wanampenda, alikuwa ni kipenzi cha kila mtu kwa kweli".

Hiyo ni sehemu tu ya mahojiano ambayo eNewz tumefanya na mastaa wengi wa muziki hususan vijana, ambao wameguswa na msiba huo kwa namna moja ama nyingine.