Wednesday , 20th May , 2015

Msanii wa Hip Hop hapa Bongo, Wakazi amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa wasanii kuendelea kufanya Albam na pia mixtape, na pia mchango wao kutambulika kwa upande wa tuzo za muziki ambazo zinatolewa hapa Tanzania.

msanii wa miondoko ya Hip Hop nchini Wakazi

Wakazi amesema kuwa endapo muamko utaongezeka na wasanii wataendelea kutoa albam na pia mixtape, uelewa utaongezeka na kuwezesha pia kazi zao kutambulika na katika tuzo pia kuongezeka kwa vipengele muhimu vya albam bora na mixtape bora.

Star huyo ambaye mpaka sasa ana jumla ya mixtape 5, amekazia kuwa kuendelea kutoa mixtape kwa upande wake na kwa wasanii kwa ujumla kunamsaidia kufanya mazoezi na kutambua rekodi zinazopendwa.