Monday , 18th May , 2015

Burudani kali ya muziki wa 'LIVE' imechukua nafasi yake mwishoni mwa wiki kupitia onesho la muziki wa Hisia ambalo limefanyika Dar kwa mara ya kwanza kabisa, na kuwa kivutio kwa umati mkubwa wa watu wakiwepo mastaa mbalimbali wa muziki.

mwanamuziki wa miondoko ya Soul na RnB wa nchini Tanzania Hisia

Kivutio cha aina yake kilikuwa ni maonesho ya msanii Heri Muziki, Grace Matata, Damian Soul vilevile AY na Banana ambao walipanda jukwaani kuongezea ladha kabla ya nyota mwenye show hiyo Hisia kupanda jukwaani na kutumbuiza.

eNewz kutoka eneo la tukio tukapata nafasi ya kuongea na baadhi ya mastaa hao, na Hisia mwenyewe kuhusu show hiyo na vilevile muziki wa'LIVE' kwa ujumla hapa Bongo.