Wednesday , 4th Jun , 2014

Mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wametoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mtayarishaji Vipindi na Muongoza Filamu maarufu nchini Tanzania marehemu George Tyson katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.

Shughuli hiyo iliyohudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa DSM Said Meck-Sadik na viongozi wa kisiasa pamoja na wadau wa filamu.

shughuli hiyo ya kuaga imefanyika kwa lengo la kuwapatia fursa watu na wadau wa filamu, ndugu na jamaa kumuaga mpendwa wao Tyson kwa upande wa Tanzania kabla ya kumsafirisha kuelekea nchini Kenya ambapo ndipo maziko yatakapofanyika.

Huzuni, vilio na simanzi zilitanda katika viwanja hivyo vya Leaders Club wakati mwili wa Tyson ulipoletwa na wakati wa kutoa heshima za mwisho.

Mwili wa marehemu utasafirishwa kwa ndege kuelekea huko Kenya ambapo maziko yatafanyika siku ya Jumamosi tarehe 14 mwezi huu.

Mungu ailaze roho ya Marehemu George Tyson Mahala Pema Peponi. Amen.