Tuesday , 25th Aug , 2015

Video ya kolabo ya kimataifa ya staa wa muziki Octopizzo kutoka Kenya na August Alsina kutoka Marekani ya “This Could Be Us” hatimaye imetoka rasmi, maoni mengi ya mashabiki yakionyesha kutokuridhishwa na kazi hiyo.

Staa wa muziki wa nchini Kenya Octopizzo na rapa nyota wa Marekani August Alsina

Kwa mujibu wa wachambuzi, Video hiyo mbali na ubora wake,kikubwa kikiwa ni kutoonekana kwa August mwenyewe na kunakiliwa kwa baadhi ya shoti za kamera baadhi ya sehemu zimenakiliwa kutoka video ya Loyal ya Chris Brown, kipande anachoonekana akicheza na mto kitandani pia kikiwa ni wazo lililotumika katika video nyingi za muziki.

Ngoma hii ya Octopizzo hata hivyo imeweza kuvutia macho ya watu wengi tangu ilipovuja miezi 9 iliyopita na kujenga matarajio makubwa ya video yake, na vilevile kwa muziki wa msanii huyo kwa ujumla.