Thursday , 21st May , 2015

Kutoka kanda ya kaskazini, msanii kutoka kundi la Vatoloco Soldiers, Fido Vato amesema kuwa wamejipanga kusogeza muziki wao karibu zaidi na mashabiki wao, wakiwa na mkakati wa kujenga studio ndani ya jiji la Dar es Salaam.

staa wa muziki wa Hip Hop anayetokea Arusha Fido Vato

Rapa huyo mkali wa mistari amewaweka wazi mashabiki wake kuwa njia hiyo itawasaidia kufikia mashabiki wengi zaidi.

Fido ameiambia eNewz kuwa, mkakati huo tayari umekwishaanza na ana imani kubwa kuwa studio hiyo ikishakamilika, kazi zao nyingi zitakuwa zikifanyika hapa jijini na hivyo kuwafikia mashabiki kwa ukaribu zaidi.