Friday , 14th Feb , 2014

Vanessa Mdee, msanii wa muziki ambaye nyota yake inang'ara vizuri kabisa hapa Bongo, amesema kuwa katika siku hii ya Wapendanao, Valentine wake ni mashabiki wake wote wa karibu ambao amekuwa karibu nao na kuonyeshana nao upendo hususan kupitia njia ya mitandao ya kijamii.

Msanii huyu amesema kuwa, anawapenda sana mashabiki wake kama ambavyo anaamini kuwa wanampenda pia, na katika ujumbe wake wa siku hii amewataka kuendeleza upendo kila siku bila kupunguza, kama ambavyo mwenyewe anasema 'keep the vibe on'.

Vanessa pia amewataka wapenzi wa muziki wake kukaa tayari video ya ngoma yake kali kabisa ya Come Over, na pia ngoma nyingine mpya kutoka kwake, ambayo itatoka mapema mwezi wa tatu mwaka huu huku akitaka watu kufahamu kuwa, "she now very seriously into music".