
Vanessa Mdee na Chris Brown
Bongo Fleva diva Vanessa Mdee ametuhabarisha kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kuwa, amepata mfuasi mpya ambaye ni Chris Brown.
Vanessa aliandika kuwa Chris Brown amem-follow kupitia mtandao huo na kusema, "wote mnajua jinsi gani ninavyomkubali huyu jamaa, Chris Brown ameni-follow mimi".
Vanessa Mdee ni mmoja kati ya wasanii wakubwa barani Afrika ambao wanafuasi wengi kupitia mtandao wa Instagram akiwa na wafuasi milioni 4.9.
Pia mkali wa muziki wa RnB hapa Tanzania Ben Pol, ametuhabarisha kupitia mtandao huohuo wa Instagram kuwa amekutana uso kwa uso na mfalme wa muziki wa Trap duniani T.I.
Ben Pol baada ya kukutana na staa huyo aliandika "amani na mfalme T.I", ukiachilia mbali kukutana na T.I, Ben Pol pia amekutana na staa wa filamu na mtayarishaji aitwaye Terrence J.