
Kundi la Mafya Crew ambalo lilishiriki usaili wa kwanza.
Akizungumzia shindano la kesho mratibu Bhoke Egina amesema shindano la kesho litakuwa babu kubwa kutokana na washiriki kutambua kwamba ni usaili wa mwisho hivyo ni shindano ambalo litakuwa la aina yake katika usaili wa msimu huu.
''Kesho ni usaili wa mwisho na ikumbukwe kwamba kutokana na zawadi ya mwaka huu kuongezeka hadi kufikia milioni 7 kumefanya hamasa kubwa sana hivyo watu wajitokeze kwa wingi ili kuhakikisha wanapata burudani ya aina yake na pia kutakuwa n zawadi mbalimbali kwa watazamaji'' Amesema Bi Bhoke.
Aidha makundi matano yatakayopatikana kesho yataanza mazoezi pamoja na makundi mengine 10 ya usaili wa kwanza na wa pili katika kusaka mshindi wa nafasi ya robo fainali, nusu fainali na fainali yenyewe.
Shindano hili linaoneshwa na EATV kila siku ya Jumapili kuanzia saa moja kamili jioni kwa udhamini wa Vodacom na Coca-Cola.
