Tuesday , 7th Oct , 2014

Msanii mahiri wa filamu , Tyler Perry kutoka Marekani anatarajia kutua nchini Kenya mwezi Novemba mwaka huu kwa ajili ya kushiriki katika mkutano wa Kimataifa wa masuala ya uongozi.

Muigizaji wa nchini Marekani Tyler Perry

Tyler katika ujio huo, kwa hadhi na nafasi yake atahamasisha na kufundisha umati mkubwa unaotarajiwa kuhudhuria mkutano huo juu ya mbinu za mafanikio.

Mkutano huo wenye utaratibu wa kualika watu mashuhuri, safari hii umejitengenezea sifa kwa kuzingatia sekta ya Burudani kwa ujio wa Perry ambaye atakuwa na mchango wa aina yake kwa wadau na wasanii kulielewa zaidi soko la filamu kimataifa.