Thursday , 1st May , 2014

Wabunifu mitindo ya mavazi Twins fashions ambao pia wanafanya kazi ya kuwavalisha wasanii wa muziki hapa Tanzania, wameelezea furaha yao kutokana na mafananikio waliyoyapata.

Wabunifu mitindo ya mavazi ambao wameibukia kwa kasi kubwa katika tasnia hiyo, Twins fashions ambao pia wanafanya kazi ya kuwavalisha wasanii wa muziki hapa Tanzania, baada ya mafanikio makubwa ya kuvalisha wasanii wakubwa, wamesema wanajivunia kufanya kazi hiyo.

Twins Fashion mpaka sasa wanashikilia rekodi ya kuwavalisha wasanii kama Makomandoo na Diamond Platinumz, wamezunguzia safari yao katika ubunifu mpaka kufika hatua waliyopo sasa.

Twins Fashion wamesema kuwa, safari ya kuanza kubuni mitindo ya mavazi kwaajili ya wasanii imechukua muda mrefu sana ikiwa na changamoto nyingi, ikiwemo wasanii hawa kutokuwa wanawaelewa na wala kukubali kazi zao katika siku za mwanzoni, mpaka sasa ambapo kazi zao zimeanza kufahamika na kupata mafanikio makubwa.

Mmoja wa wabunifu hawa kutoka Twins Fashion, Johnson anazungumza kwa kifupi juu ya safari yao.